// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YULE KOCHA WA SIMBA APATA KAZI KENYA TENA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YULE KOCHA WA SIMBA APATA KAZI KENYA TENA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, February 13, 2015

    YULE KOCHA WA SIMBA APATA KAZI KENYA TENA

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    AFC Leopards ya ligi kuu ya taifa la Kenya imemteua aliyekuwa kocha wa Simba SC na Mcroatia Zdravko Logarusic kama kocha mkuu siku chache tu kabla ya msimu wa 2015 kuanza.
    Logarusic anachukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mholanzi Hendrik Pietter De Jongh aliyepigwa kalamu baada ya msimu jana kwa kile viongozi wa mabingwa hao mara 12 Kenya walikitaja kama ukosefu wa stakabadhi muhimu za ukufunzi.
    Logarusic kwa mjibu wa naibu katibu mkuu Prof. Asava Kadima, anachukua majukumu hayo wakati wowote toka sasa na anatarajiwa kuzinduliwa mapema wiki ijayo.
    Zdravko Logarusic amepata kazi tena Kenya, baada ya kuondoka Simba SC

    Kocha huyo mwenye vishasha na mbwembe nyingi uwanjani si mgeni nchini Kenya kwani ashawahi kuifunza mahasimu wa Leopards, Gor Mahia tangia mwaka 2012 kabla ya kujiunga na Simba SC Desemba 2013 baada ya kuonyeshwa mlango.
    Mikosi ya kutupwa inje ilizidi kumwandama nchini Tanzania kwani Wekundu hao wa Msimbazi walimtupia virago mwezi Agosti 2014.
    Amekuwa bila timu tangia hapo na sasa atasaidiwa na kocha wa zamani wa Coastal Union ya Tanga, Yusuf Chippo.
    Leopards imekita kambi katika makao yao makuu mjini Mumias, magharibi mwa Kenya tangu Alhamisi. Mechi ya kwanza ya Loga kwenye ligi kuu itakuwa jumamosi tarehe 21 Februari dhidi ya Chemelil Sugar uwanjani Chemelil.
    Katika habari zingine, katibu katika wizara ya michezo Daktari Hassan Wario anatarajia kukutana na viongozi wa Shirikisho la Soka, FKF, na kampuni inayosimamia ligi kuu, KPL, siku ya jumatatu 16 Februari kusuluhisha tofauti iliyoko baina yao kuhusu idadi ya timu za ligi kuu msimu wa 2015.
    FKF inazitaka timu 18 huku KPL na wafadhili wake Tusker na SuperSport wakisisitiza timu 16 na sasa Wario anamatumaini ya kupata maafikiano katika mkutano huo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YULE KOCHA WA SIMBA APATA KAZI KENYA TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top