// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA TIENI VICHWA MAJI; PLATINUM HAOOO WAIVAA SOFAPAKA KENYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA TIENI VICHWA MAJI; PLATINUM HAOOO WAIVAA SOFAPAKA KENYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 15, 2015

    YANGA TIENI VICHWA MAJI; PLATINUM HAOOO WAIVAA SOFAPAKA KENYA

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    FC PLATINUM ya Zimbabwe imetuma onyo la mapema kwa wapinzani watarajiwa Yanga SC katika raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika kwa kuivaa Sofapaka ya Kenya 2 – 1 kwenye mechi za mkondo wa awali uwanjani Nyayo, Nairobi alasiri ya leo.
    Huenda Yanga ikamenyana na klabu hiyo ya Zimbabwe iwapo timu zote mbili zitapigilia msumari wa mwisho kwenye ushindi wao katika mechi za marudiano majumaa mawili yajayo baada ya Yanga kuwafumua BDF XI jana Taifa.

    Magoli ya Platinum yalifungwa na Brian Muzondiwa mnano dakika ya 25 kisha Donald Ngoma akapiga la pili dakika ya 74. Raia wa Burundi Fiston Abdoul Razak alikuwa amewapa vijana wa Sam Timbe bao lao la kipekee dakika ya 47.
    Muzondiwa alimalizia pasi ya Wisdom Mutasa huku Ngoma akiunganisha pasi murwa ya Walter Musona baada ya kipa wa Sofapaka David Okello kuzidiwa na ujuzi wa kupangua krosi hiyo.
    Platinum ilionyesha mchezo wa kasi uliyowazidi Batoto ba Mungu na ili kufuzu, Sofapaka itahitaji angalau ushindi wa magoli mawili kwa nunge, jambo ambalo kocha Timbe ana imani nalo.
    “Huu ni mpira chochote chawezekana popote, nakumbuka miaka ya hapo awali Simba walipigwa 6 – 0 na timu fulani kutoka Zambia mkondo wa kwanza nao wazambia wakalazwa magoli yayo hayo mechi ya marudiano,” alisema Mganda huyo baada ya mechi.
    Mpinzani wake Norman Mapeza naye alijipiga kifua kwa kuvuna ushindi muhimu na kuihakikishia Sofapaka mchezo mwingine nyumbani.
    “Nimefurahi na ushindi ugenini lakini hamjaona mchezo wa kitabu akili na ubongo, ngojeni mechi ya marudiano,” alisema Mapeza.
    Mechi ya marudiano imeratibiwa tarehe 27 Februari uwanjani Mandava mjini Zvishavane, Zimbabwe.
    Kikosi cha Sofapaka kilikuwa: 29 David Okello, 6 Shafique Batambuze, 8 Willis Ouma, 15.John Bagoole, 5 Felly Mulumba, 14 Ekhaliana Ndolo, 13 Danson Kago, 24 Maurice Odipo, 25 Enock Agwanda/12 John Baraza, (dk 87’), 22 Abduol Fiston, 10 Patrick Kagogo/20 Kevin Omondi (dk 69)
    Kikosi cha FC Platinum kilikuwa: 1. Petros Mhari (GK), 15. Gift Bello, 24. Moyo 7. Raphael Muduviwa, 21. Kevin Moyo, 8. Tatenda Dzumbunu/4. Simon Shoko (dk 76’) 10. Wisdom Mutasa/6. Wellington Kumudiyariwa (dk 72’) 13. Thabani Kamusoko (CPT), 11. Donald Ngoma, 20. Brian Muzondiwa, 17. Walter Musona
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA TIENI VICHWA MAJI; PLATINUM HAOOO WAIVAA SOFAPAKA KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top