// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC WAHENYESHWA NA NDANDA 0-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC WAHENYESHWA NA NDANDA 0-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 01, 2015

    YANGA SC WAHENYESHWA NA NDANDA 0-0

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    YANGA SC wameendelea kuonyesha 'ufundi' wa kukosa mabao ya wazi jioni ya leo wakilazimishwa sare ya bila kufungana na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Martin Saanya wa Dar es Salaam aliysaidiwa na Sophia Mtongori wa Mara na Charles Simon wa Dodoma, dakika ya 10 Mrisho Ngassa alimpa pasi nzuri Simon Msuva, lakini akapiga shuti dhaifu likadakwa na kipa Albvert Mweta.
    Dakika ya 13 Ngassa alishindwa kufunga katikati ya msitu wa mabeki wa Ndanda baada ya pasi ya Salum Telela.
    Dakika ya 15 Masoud Ally wa Ndanda alipiga nje akiwa umbali wa mita chache na kuikosesha timu yake bao.
    Beki wa Yanga SC, Juma Abdul akiwaacha mabeki wa Ndanda, Ernest Mwalupani aliyekaa chini na Paul Ngalema nyuma yake
    Winga wa Yanga SC, Simon Msuva akipambana na beki wa Ndanda, Paul Ngalema

    Dakika ya 24 Danny Mrwanda alipiga kichwa dhaifu baada ya krosi ya Msuva kipa akadaka na dakika ya 30, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alipaisha kwa shuti baada ya kona ya Msuva.
    Dakika ya 51 Kpah Sherman aligongesha mwamba krosi ya Msuva na akaenda moja kwa moja kukagua langoni mwa Ndanda baada ya kukosa bao hilo, kabla ya kupewa kadi ya njano kwa kujiangusha ndani ya boksi dakika chache baadaye. Mrwanda naye akiwa peke yake ndani ya sita akapiga juu wakati kipa amekwishatoka langoni dakika ya 76.
    Dakika ya 89, Ernest Mwalupani alipewa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu kwa kuchelewa kupiga mpira.
    Kikois cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Hassan Dilunga/Said Juma ‘Kizota’, Kpah Sherman/Tambwe, Dan Mrwanda na Mrisho Ngassa/Jerry Tegete.
    Ndanda FC; Wilbert Mweta, Aziz Sibo, Paul Ngalema/Shukuru Chachala, Cassian Ponela, Ernest Mwalupani, Zabron Raymond/Kiggi Makassy, Jacob Massawe, Omega Seme, Nassor Kapama, Stahmili Mbonde na Masoud Ally/Rajab Isihaka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAHENYESHWA NA NDANDA 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top