// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC SAFARI MBEYA MECHI MBILI ‘DABO’, WAKIRUDI TU WANAUNGANISHA GABORONE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC SAFARI MBEYA MECHI MBILI ‘DABO’, WAKIRUDI TU WANAUNGANISHA GABORONE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 15, 2015

    YANGA SC SAFARI MBEYA MECHI MBILI ‘DABO’, WAKIRUDI TU WANAUNGANISHA GABORONE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Yanga SC kinaondoka Alfajiri ya kesho Dar es Salaam kwa basi lao kubwa, kuelekea Mbeya kwa ajili ya mechi na wenyeji Prisons Alhamisi.
    Yanga SC watateremka Uwanja wa Sokoine, Mbeya katikati ya wiki kusaka pointi tatu dhidi ya timu hiyo ngumu inayomilikiwa na jeshi la Magereza katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Baada ya mchezo huo, Yanga SC watashuka tena Uwanja wa Sokoine kumenyana na wenyeji wengine, Mbeya City Jumapili katika mfululizo wa ligi hiyo. 

    Yanga SC wanakwenda Mbeya, wakitoka kuanza vizuri mechi ya kwanza Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuifunga BDF XI ya Botswana mabao 2-0 jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Na wakitoka Mbeya tu, wataunganisha safari hadi Gaborone kwa ajili ya mchezo wa marudiano na BDF. 
    Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm bado na mtihani wa kufanyia kazi mapungufu ya safu yake ya ushambuliaji ambayo inashindwa kutumia nafasi nyingi inazotengeneza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC SAFARI MBEYA MECHI MBILI ‘DABO’, WAKIRUDI TU WANAUNGANISHA GABORONE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top