// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC HATARINI KUMKOSA ‘KAPTENI’ CANNAVARO DHIDI YA BDF JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC HATARINI KUMKOSA ‘KAPTENI’ CANNAVARO DHIDI YA BDF JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 12, 2015

    YANGA SC HATARINI KUMKOSA ‘KAPTENI’ CANNAVARO DHIDI YA BDF JUMAMOSI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KOCHA mkuu wa Yanga Hans van der Pluijm amesema kwamba Nahodha wake, Nadir Haroub 'Cannavaro' yuko kwenye hatihati ya kucheza mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana Jumamosi.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo Dar es Salaam, Pluijm amesema ukiacha shaka hiyo juu ya Cannavaro, kila kitu kuhusu timu yake kipo sawa ambapo anazidi kufurahia umoja, mshikamano na utulivu waliokuwa nao vijana wake.
    Pluijm amesema wapo tayari kwa kila kitu kuhusu wapinzani wao hao, lakini hofu yao ni maumivu aliyokuwa nayo Cannavaro ambaye goti lake la kulia.
    Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' anasumbuliwa na maumivu ya goti
    Kocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm hana wasiwasi na BDF 

    "Hatujajua kama atakuwa sawa mpaka siku ya mchezo ni jambo la kusubiria leo na kesho kuangalia maendeleo yake lakini tunaimani atakuwa sawa, mbali na hapo naweza kusema tupo tayari kuingia vitani kupambana na hao Wanajeshi,"amesema Pluijm.
    Wakati huo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga Jerry Muro amesema tayari wameanza kuuza tiketi za mchezo huo dhidi ya BDF ambao wanatua leo jioni na ndege maalum ya jeshi la Botswana.
    "Wapinzani wetu wanaingia leo na ndege maalum ya jeshi la kwao na waankuja na msafara qwa wachezaji 25 pamoja na viongozi wao tunaomba wale wote wanaoipenda Yanga kununua tiketi mapema kuanzia leo ili kupunguza msongamano siku ya mchezo na siku hiyo milango ya Uwanja itafunguliwa mapema kuanzia saa saba mchana,"alisema Murro.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC HATARINI KUMKOSA ‘KAPTENI’ CANNAVARO DHIDI YA BDF JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top