// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA PUMBA, AU MCHELE AFRIKA? TUTAJUA LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA PUMBA, AU MCHELE AFRIKA? TUTAJUA LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, February 14, 2015

    YANGA PUMBA, AU MCHELE AFRIKA? TUTAJUA LEO

    Na Mwandishi Wetu, CAIRO
    MECHI ZA mchujo za Kombe la Shirikisho Afrika zinaanza wikiendi hii, vigogo wa Tanzania, Yanga SC wakiwakaribisha BDF XI ya Botswana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Jumla ya timu 55 zipo kwenye michuano hii, lakini 
    Zamalek ya Misri, Orlando Pirates ya Afrika Kusini, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Djoliba ya Mali, FUS Rabat ya Morocco, AS Vita ya DRC, Ahly Shandy ya Sudan na timu mbili za Tunisia, Club Africain na Etoile du Sahel zitaanzia hatua ijayo.
    Mjini Dar es Salaam, makocha wa timu za Yanga na BDF zitakazomenyana leo walifanya Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wao.
    Kocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm alisema BDF ni timu nzuri na mchezo utakuwa mgumu.
    Yanga SC watakuwa wenyeji wa BDF XI ya Botswana leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    Hata hivyo, Mholanzi huyo alisema kwamba Yanga imejiandaa kikamilifu kushinda mchezo huo.
    Kocha wa BDF, Letang Kgengwenyane, amesema kwamba tofauti na timu nyingine zinazokwenda ugenini bila malengo ya kushinda, wao wametua Dar kupigni ushindi na hawatajilinda kutafuta sare.
    "Imezoeleka kwamba timu inapocheza ugenini inatumia mfumo wa kujilinda, kwetu ni tofauti tutashambulia kwa nguvu, lakini pia tutazuia, tunataka kusonga mbele, ni lazima tupate mabao, tumefanya maandalizi ya kutosha tangu tulipopata nafasi ya kushiriki kombe hili,"alisema Kgengwenyane.
    Mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, Mrisho Khalfan Ngassa amejiandaa kikamilifu akiwa katika kiwango cha juu kuelekea mchezo wa leo.
    Ngassa amenunua kiatu maalum kwa ajili ya BDF chenye jina lake, kilichotengenezwa na Kampuni ya Nike ambayo pia ndiyo wadhamini wakuu wa mshambuliaji wa Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo kimeshatua kikitokea nchini Uingereza.
    Ngassa aliiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba amelazimika kutumia kiasi cha Sh 300,000 kuagiza kiatu hicho ambacho ubavuni kimeandikwa jina lake na namba 17 anayotumia katika timu hiyo.
    "Niliwaza nifanye nini katika mchezo huu, nikapanga kwamba nataka kuisaidia Yanga katika mechi zake hususan hizi mechi za Kimataifa ambazo msimu uliopita nilikuwa mfungaji bora,"alisema Ngassa.
    "Mbali na hilo nikapata wazo la kutafuta kiatu maalum kama ambavyo wenzetu wa Ulaya wanafanya nikaona niagize kiatu Uingereza kilichoandikwa jina langu na sasa kimefika nikipata nafasi kesho (leo) watu watakiona,".
    URA ya Uganda wataikaribisha ASSM Elgeco ya Madagascar mjini Kampala, Uganda


    RATIBA MECHI ZA MCHUJO KOMBE LA SHIRIKISHO
    Jana, Februari 13, 2015
    Renaissance Berkane (Morocco) Vs Onze Createurs (Mali)
    Al Ghazala (Sudan Kusini) Vs Petrojet (Misri)
    Benfica Luanda (Angola) Vs Le Messager de Ngozi (Burundi)
    Leo, Februari 14, 2015
    Yanga SC (Tanzania) Vs BDF XI (Botswana)
    URA (Uganda) Vs ASSM Elgeco (Madagascar)
    Mouloudia Alger (Algeria) Vs Sahel SC (Niger)
    Leones Vegatarianos Leones (Equatorial Guinea) Vs Dolphins (Nigeria)
    Cote d'Or (Shelisheli) Vs Dedebit (Ethiopia)
    RC Bobodioulasso (Burkina Faso) Vs Warri Wolves (Nigeria)
    Etoile du Congo (Kongo) Vs FC MK (DRC)
    Panthere Nde (Cameroon) Vs Rayon Sports (Rwanda)
    Al-Khartoum (Sudan) Vs Power Dynamos (Zambia)
    Volcan de Moroni (Comoro) Vs Petro Atletico (Angola)
    Bidvest Wits (Afrika Kusini) Vs Royal Leopards (Swaziland)
    Petite Riviere Noire (Mauritius) Vs Ferroviario Beira (Msumbiji)
    Kesho, Februari 15, 2015
    Al Ittihad (Libya) Vs Elect Sport (Chad)
    UFC de Haut Nkam (Cameroon) Vs Olympique Ngor (Senegal)
    Hearts of Oak (Ghana) Vs Police (Benin)
    ASO Chlef (Algeria) Vs Kamboi Eagles (Sierra Leone)
    Horoya (Guinea) Vs Fassell (Liberia)
    AS Port (Togo) Vs CARA (Kongo)
    CF Mounana (Gabon) Vs Polisi (Zanzibar)
    Sofapaka (Kenya) Vs Platinum (Zimbabwe)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA PUMBA, AU MCHELE AFRIKA? TUTAJUA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top