Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
CHAMA cha Soka Dar es Salaam (DRFA), kimetaja makundi ya timu zitakazoshiriki kucheza hatua ya 18 bora (hatua ya pili) ya Ligi ya mkoa wake inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi baadaye mwezi huu.
Katika kundi (A) limepangwa kuwa na timu za Simba U20, Red Coast, Sifa United, Shababi, Ukonga United, Zakhem, Ugimbi, Beira Hotspur na Pan Africa.
Kundi B litakuwa na timu za Yanga U20, Stakishari, FFU, New Kunduchi, Sinza Stars, Changanyikeni, Tuamoyo, Sifapilitan na Azania Unga.
Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36, imeingia katika hatua ya pili, ambayo itaanza Februari 11 mwaka huu katika viwanja mbalimbali.
Kundi A Simba U20 itamenyana na Red Coast, Uwanja wa Karume, Sifa United na Shababi Uwanja wa Mwalimu Nyerere, Ukonga United na Zakhem Uwanja wa Airwing, Ugimbi na Beira Hotspur Uwanja wa Bandari.
Kundi B Februari 12, Yanga U20 itacheza na Stakishari Karume, FFU na New Kunduchi Benjamini Mkapa, Sinza Stars na Changanyikeni Kinesi na Tuamoyo na Sifapolitan Bandari.
Viongozi wa DRFA bado wanatoa wito kwa viongozi wa vilabu mbalimbali, mashabiki na wakazi wa jiji pamoja na maeneo ya jirani, kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya wachezaji.

Kikosi cha Simba B kilochokuwa tishio miaka mitatu iliyopita, ambacho asilimia kubwa ya wachezaji wake wamepandishwa kikosi cha kwanz cha timu hiyo hivi sasa |
Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36, imeingia katika hatua ya pili, ambayo itaanza Februari 11 mwaka huu katika viwanja mbalimbali.
Kundi A Simba U20 itamenyana na Red Coast, Uwanja wa Karume, Sifa United na Shababi Uwanja wa Mwalimu Nyerere, Ukonga United na Zakhem Uwanja wa Airwing, Ugimbi na Beira Hotspur Uwanja wa Bandari.
Kundi B Februari 12, Yanga U20 itacheza na Stakishari Karume, FFU na New Kunduchi Benjamini Mkapa, Sinza Stars na Changanyikeni Kinesi na Tuamoyo na Sifapolitan Bandari.
Viongozi wa DRFA bado wanatoa wito kwa viongozi wa vilabu mbalimbali, mashabiki na wakazi wa jiji pamoja na maeneo ya jirani, kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya wachezaji.
0 comments:
Post a Comment