// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA KUMKOSA BEKI WAKE MAHIRI DHIDI YA BDF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA KUMKOSA BEKI WAKE MAHIRI DHIDI YA BDF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 09, 2015

    YANGA KUMKOSA BEKI WAKE MAHIRI DHIDI YA BDF

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA SC itamkosa beki wake mahiri chipukizi, Edward Charles Manyama katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana mwishoni mwa wiki.
    Edward alitoka nje dakika ya 39 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bada jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kuumia enka na nafasi yake ikichukuliwa na Juma Abdul.
    Na leo Daktari wa Yanga SC, Juma Sufiani amesema mlinzi huyo wa pembeni kushoto atakuwa nje kwa siku 10 akiuguza maumivu yake, maana yake Jumamosi atakosekana.
    Edward Charles jana baada ya kuumia

    Lakini hapana shaka kuumia hadi kukosekana kwa beki huyo aliyesajiliwa msimu huu kutoka JKT Ruvu si pigo sana, kwa sababu yupo beki chaguo la kwanza katika nafasi hiyo, Oscar Fanuel Joshua.
    Kuna uwezekano Charles akaukosa hata mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho, lakini hakuna shaka mapema Machi atakuwa fiti kabisa kuanza tena kufanya kazi Jangwani.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA KUMKOSA BEKI WAKE MAHIRI DHIDI YA BDF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top