BAO la dakika za lala salama la Willian, limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Everton usiku huu katika mcheo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Toffees walifungwa bao hilo baada ya kumpoteza mchezaji wake, Gareth Barry aliyetolewa kwa kadi nyekundu na sasa The Blues wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi saba zaidi.
Steven Naismith alikuwa mwenye bahati baada ya kuepuka adhabu licha ya kuunawa mpira kwenye boksi la Everton kipindi cha kwanza.
Kiungo mpya, Juan Cuadrado alianza kwa amra ya kwanza leo tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 27 Chelsea kutoka Fiorentina na akavutia.
Willian akishangilia na Didier Drogba baada ya kufunga
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2949817/Chelsea-1-0-Everton-Willian-leaves-late-break-10-man-Toffees-Gareth-Barry-sees-red.html#ixzz3RTcs8XE3
0 comments:
Post a Comment