// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAPINZANI WA YANGA WAJA KESHO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAPINZANI WA YANGA WAJA KESHO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, February 11, 2015

    WAPINZANI WA YANGA WAJA KESHO DAR

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    WAPINZANI wa Yanga SC, BDF XI wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Alhamisi kuelekea mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho la Afrika Jumamosi.
    Yanga SC watacheza na BDF XI Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho wakihitaji ushindi mzuri kujiweka katika mazingira mazuri kabla ya mchezo wa marudiano baadaye Gaborone.
    Na wapinzani wao hao ambao awali ‘walizusha’ eti wamejitoa, watawasili kesho Dar es Salaam huku ikiwa bado haijajulikana watafikia hoteli gani- kwa sababu ya taratibu mpya za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

    CAF sasa imeamua timu zijilipie malazi zinapokwenda kwenye mechi za ugenini baada ya kuwapo malalamiko timu ngeni kupatiwa hoteli duni miaka ya nyuma.
    Yanga SC imeweka kambi katika hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam tangu juzi kujiandaa na mchezo huo. 
    Refa wa mchezo huo atakuwa Thierry Nkurunziza, wasaidizi wake Ramadhani Nijimbere namba moja, Herve Kakunze namba mbili na mezani George Gatogato, wote wa Burundi wakati Kamisaa atakuwa Joseph Nkole wa Zambia.
    Kiingilio cha chini kabisa katika mchezo huo kitakuwa Sh. 5,000, wakati viingilio vingine vitakuwa Sh 10,000, 15, 000, 20, 000 na 30,000.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAPINZANI WA YANGA WAJA KESHO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top