Baadhi ya wachezaji wa Uganda wanaocheza Kenya, kutoka kushoto Aziz Kemba, Matthew Odongo, Ali Kimera, Hamza Muwonge
Na Vincent Malouda, NAIROBI
JUMLA ya wachezaji 26 wenye uraia wa Kiganda wamehamia ligi kuu ya taifa la Kenya kusaka posho.
Katika vilabu 14 vilivyodhibitisha vifaa vyao vya msimu wa 2015, ni viwili tu ambavyo havikuwasajili wachezaji wa Uganda navyo ni Mathare United na Chemelil Sugar.
Vigogo AFC Leopards na Gor Mahia ni baadhi ya vilabu vilivyo na zaidi ya wachezaji wawili kutoka nchi jirani ya Uganda. Kampuni inayosimamia ligi kuu, KPL, inaruhusu kila klabu kusajili wachezaji wageni wasaba lakini ni watano tu wanaoruhusiwa kuwa uwanjani wakati wa mechi.
Sheria hiyo ni mpya kwani hadi msimu uliyopita kila klabu ingewasajili wachezaji wasita tu huku watano wakiwa uwanjani kwenye ngarambe moja.
Hata hivyo, wachezaji wasaba ni wapya katika ligi kuu baada ya kusajiliwa katika dirisha la uhamisho la mwezi Desemba hadi Januari.
Nao ni Aziz Kemba, Matthew Odongo na Daniel Oryiwoth wanaowajibikia Tusker FC, David Bagoole (Sofapaka FC), Bernerd Agele (KCB FC), Ali Kimera (Ushuru FC) na Karim Nduggwa wa AFC Leopards.
Kwenye ligi ya daraja la pili, kunao zaidi ya ishirini tena kutoka Uganda wakiwemo Jimmy Bageya, Ivan Anguyo, Sula Bagala, Issaac Mutanga (Nakumatt FC), David Bogere na Patrick Senfuka (Bidco United) miongoni mwa wengine.
0 comments:
Post a Comment