WAWAKILISHI wa upande wa pili wa Tanzania katika michuano ya Afrika, KMKM na Polisi za Zanzibar wote wameanza vibaya baada ya kufungwa ugenini leo.
KMKM imefungwa mabao 2-0 na Al-Hilal ya Sudan mjini Khartoum leo Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Polisi imefungwa mabao 5-0 na CF Mounana nchini Gabon katika Kombe la Shiriksiho, zote zikiwa mechi za kwanza Raundi ya Awali michuano hiyo.
KMKM sasa itatakiwa kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo visiwani Zanzibar, wakati Polisi inatakiwa kushinda 6-0 ili zifuzu hatua ya 32 Bora.
Wawakilishi wa Bara, Azam FC na Yanga SC wote wameanza vizuri katika mechi zao za kwanza Raundi ya Awali, zote zikishinda 2-0 nyumbani.
Yanga SC walianza kuifunga BDF XI ya Botswana mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana yote yakifungwa na Mrundi, Amisi Tambwe kabla ya leo mabao ya Mrundi mwingine Didier Kavumbangu na mzalendo John Bocco kuipa Azam ushindi wa 2-0 dhidi ya Merreikh ya Sudan Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Jijini.
Sasa, timu hizo za Bara zitatakiwa kwenda kulazimisha sare ugenini wiki ijayo ili kufuzu 32 Bora ya michuano ya Afrika.

KMKM wamefungwa 2-0 na Al Hilal nchini Sudan leo |

0 comments:
Post a Comment