// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAWAPIGIA ‘SALUTI’ TEMBO WA IVORY COAST - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAWAPIGIA ‘SALUTI’ TEMBO WA IVORY COAST - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, February 10, 2015

    TFF YAWAPIGIA ‘SALUTI’ TEMBO WA IVORY COAST

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Sidy Diallo wa Shirikisho la Soka Ivory Coast (FIF) kwa kutwaa Ubingwa wa Mataifa Afrika.
    Katika salamu, Malinzi amesema mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa wa Afrika yametokana na juhudi za Rais huyo pamoja na Kamati yake ya Utendaji.
    “Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi Shirikisho la mpira wa Miguu la Ivory Coast kwa kutwaa Ubingwa huo wa Afrika kwa mara pili,”.

    Aidha, Malinzi amempongeza Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou kwa kufanikiwa kuandaa salama fainali za Mataifa Afika Equatorial Guinea pamoja na hofu ya ugonjwa wa Ebola.
    Katika salamu hizo kwenda kwa Haytou na nakala yake kupitia Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Hicham El Amrani, Malinzi amesema kwa pamoja analipongeza Shirikisho hilo na wenyeji wa michuano kwa kufanikiwa kuandaa mashindano hayo na kumalizika salama.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAWAPIGIA ‘SALUTI’ TEMBO WA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top