// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAIWEKEA NGUMU YANGA SC, MECHI YAO NA MTIBWA SUGAR KUPIGWA JUMAPILI TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAIWEKEA NGUMU YANGA SC, MECHI YAO NA MTIBWA SUGAR KUPIGWA JUMAPILI TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 05, 2015

    TFF YAIWEKEA NGUMU YANGA SC, MECHI YAO NA MTIBWA SUGAR KUPIGWA JUMAPILI TAIFA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limekataa ombi la Yanga SC kutaka mchezo wao na Mtibwa Sugar uahirishwe ili wapate fursa nzuri ya maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana.
    Na kwa sababu, hiyo Yanga SC wanaondoka asubuhi ya leo kurejea kambini kwao, Bagamoyo kuendelea na maandalizi ya mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Yanga SC watacheza mechi ya tatu ndani ya wiki moja Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya mabingwa wenzao wa zamani wa Ligi Kuu, baada ya Jumapili iliyopita kulazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC na jana kushinda 1-0 dhidi ya Coastal Union. 
    Kikosi cha Yanga SC kilichoifunga Coastal Union jana Mkwakwani

    Yanga SC ilipanda kileleni mwa Ligi Kuu jana kufuatia ushindi huo wa ugenini, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa kutimiza pointi 22 baada ya kucheza mechi 12, moja zaidi ya mabingwa watetezi, Azam FC walioteremkea nafasi ya pili kwa pointi zao 21.
    Shujaa wa pointi tatu za Yanga SC jana alikuwa ni Nahodha Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’, aliyefunga bao hilo pekee mapema tu kipindi cha kwanza, baada ya kupanda kwenda kusaidia mashambulizi. 
    Ilikuwa ni dakika ya 12 ya mchezo, wakati Cannavaro alipomalizia kwa kichwa mpira mpira wa kurushwa wa beki Mbuyu Twite na kuipandisha kileleni Yanga SC.  
    Baada ya mchezo na Mtibwa Sugar Jumapili, Yanga SC itakwenda kuweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa kwanza, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAIWEKEA NGUMU YANGA SC, MECHI YAO NA MTIBWA SUGAR KUPIGWA JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top