// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TANZANIA YAICHAPA 5-3 KENYA SOKA LA UFUKWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TANZANIA YAICHAPA 5-3 KENYA SOKA LA UFUKWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 16, 2015

    TANZANIA YAICHAPA 5-3 KENYA SOKA LA UFUKWE

    Na Mwandishi Wetu, MOMBASA
    Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni (Beach Soccer) jana imeibuka na ushindi wa mabao 5- 3 ugenini dhidi wa wenyeji timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa fukwe za Hotel ya Big Tree Pirates jijini Mombasa.
    Katika mchezo huo mabao ya Tanzania yalifungwa na Ali Rabbi mabao manne na Mwalimu Akida bao moja .
    Kipindi cha kwanza kilimazika kwa Tanzania kupata mabao 2 Kenya 1, kipindi cha pili kilimalizika Tanzania 4 Kenya 3 na kipindi cha tatu na cha mwisho kwa mchezo kUmalizika kwa Tanzania kupata mabao 5 Kenya 3.

    Mechi ya marudiano inatarajiwa kuchezwa jumamosi wiki hii Februari 21, 2015 jijini Dar es salaam, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itafanikiwa kuwatoa Kenya, itacheza na timu ya Taifa ya Misri katika hatua inayofuata.
    Mchezo wa kwanza utafanyika kati ya tarehe 7,8 Machi 2015 jiji Dar es salaam na marudiano yatafanyika nchini Misri kati ya tarehe 13,14 Machi 2015.
    Timu inarejea leo jijini Dar es salaam majira ya saa 11 jioni ikitokea jijini Mombasa nchini Kenya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YAICHAPA 5-3 KENYA SOKA LA UFUKWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top