// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA YAPIGWA KIBOKO NA FIFA KISA MOSOTI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA YAPIGWA KIBOKO NA FIFA KISA MOSOTI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 05, 2015

    SIMBA YAPIGWA KIBOKO NA FIFA KISA MOSOTI

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    Simba SC imeagizwa kumlipa beki Donald Mosoti Omanwa takribani dola za Marekani 14 400 kwa kusitisha mkataba wa mchezaji huyo raia wa Kenya mwaka jana.
    Kwenye barua ambayo BIN ZUBEIRY inaimiliki kutoka kwa Shirikisho la Soka duniani, FIFA, Simba imeagizwa kulipa fedha hizo kwa siku thelathini zijazo pamoja na riba ya asilimia tano kwa malipo yake kwa mujibu wa uamuzi uliyoafikiwa na benchi la majaji watatu; Thomas Grimm kutoka Uswizi, Eirik Monsen wa Norway na Zola Majavu kutoka Afrika Kusini.
    Donald Mosoti kushoto ameshinda kesi FIFA dhidi ya Simba SC 

    “Mshitakiwa, Simba SC, afaa kumlipa mdai, Donald Mosoti Omanwa, ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya taarifa ya uamuzi huu, malipo bora kwa kiasi cha USD 600 pamoja na 5% kama riba kwa mwaka kutoka Desemba 12, 2013,” ulisoma ujumbe uliotiwa sahihi na katibu mkuu Jerome Valcke wa korti hiyo (Dispute Resolutions Chamber).
    “Mshitakiwa pia amlipe mdai ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya taarifa ya uamuzi huu, fidia ya USD 13 800 kwa uvunjaji wa mkataba pamoja na 5% kwa mwaka riba kutoka Septemba 16, 2014hadi tarehe ya ufanisi wa malipo.”
    Hii ina maana kwamba beki huyo atatia kibindoni kitita cha zaidi ya shilingi million moja pesa za Kenya na zaidi ya milioni 19 pesa za Tanzania.

    Wekundu wa Msimbazi walimchuja Mosoti mwezi Agosti 2014 lakini mchezaji huyo akaamua kuwashitaki FIFA kupitia kwa wakili wake Felix Majani mwezi Septemba 2014.
    Kwa sasa amejiunga na klabu ya ligi kuu Kenya, Tusker FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YAPIGWA KIBOKO NA FIFA KISA MOSOTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top