// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YAICHAPA 2-0 POLISI MORO, SASA YAZIPUMULIA AZAM FC NA YANGA KILELENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YAICHAPA 2-0 POLISI MORO, SASA YAZIPUMULIA AZAM FC NA YANGA KILELENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 15, 2015

    SIMBA SC YAICHAPA 2-0 POLISI MORO, SASA YAZIPUMULIA AZAM FC NA YANGA KILELENI

    Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
    SIMBA SC imepaa hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bada kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Polisi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jioni ya leo.
    Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, washambuliaji Ibrahim Salum Hajibu na Elias Maguri, moja kila kipindi.
    Hajibu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwainua mashabiki wa Simba SC baada ya kumalizia vizuri mpira wa kurushwa na beki Hassan Kessy dakika ya 14.
    Kipindi cha pili, Maguri aliihakikishia Simba SC kuchukua pointi tatu Morogoro baada ya kufunga bao la pili dakika ya 71 baada ya beki wa Polisi kuchanganya na kipa wake.

    Kwa matokeo hayo, Simba SC inatimiza pointi 20 baada ya kucheza mechi 14 na kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nyuma ya Azam FC na Yanga SC zenye pointi 24 kila mmoja baada ya mechi 13.
    Polisi inabaki na pointi zake 19 baada ya mechi 15 na kushuka nafasi ya nne.
    Kipa Ivo Mapunda alikimbizwa hospitali baada ya kugongana na mchezaji wa Polisi na kuumia dakika ya 58 katika harakati za kuokoa langoni mwake, na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Manyika. 
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda/Peter Manyika dk58, Hassan Kessy Ramadhani/Nassor Masoud ‘Chollo’ dk83, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Mursheed, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’/Awadh Juma dk70, Abdi Banda, Elias Maguri, Ibrahim Hajibu na Emmanuel Okwi.
    Polisi Moro; Tony Kavishe, Mohammed Mpopo, Hassan Mganga, Laban Kamboole, Anafi Suleiman, Lulanga Mapunda/Said Mkangu dk68, Suleiman Kassim ‘Selembe’, James Ambrose/Nahoda Bakari dk71, Said Bahanuzi, Imani Mapunda na Christopher Edward.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA 2-0 POLISI MORO, SASA YAZIPUMULIA AZAM FC NA YANGA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top