LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwil kupigwa, huku fikra za wengi zikitekwa na mechi kati ya wenyeji Polisi dhidi ya Simba SC Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Ikitoka kutoa sare ugenini Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dhidi ya Coastal Union, Simba SC itakuwa kwenye Uwanja mwingine ‘mbovu’ leo Morogoro kusaka pointi tatu.
Kocha wa timu hiyo, Mserbia Goran Kopunvic anafahamu ugumu anaokabiliana nao leo, lakini amewaagiza wachezaji wake wapambane kuipa timu ushindi.
Kocha wa Polisi, Mohammed ‘Adolph’ Rishard kuelekea mchezo huo amesena anawaamini vijana wake wanaweza kuwapa raha wakazi wa Moro kwa kuwafunga Simba SC leo.
Simba SC yenye pointi 17 za mechi 13, ikishinda leo, itapanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nyuma ya Azam FC na Yanga SC zenye pointi 24 kila mmoja baada ya mechi 13.
Polisi yenye pointi 19 za mechi 14, nayo pia ikishinda itapanda nafasi ya tatu.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo ni kati ya Kagera Sugar watakaokuwa wenyeji wa JKT Ruvu Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

0 comments:
Post a Comment