// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA NA YANGA B ZATINGA 18 BORA LIGI YA MKOA DAR ES SALAAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA NA YANGA B ZATINGA 18 BORA LIGI YA MKOA DAR ES SALAAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 01, 2015

    SIMBA NA YANGA B ZATINGA 18 BORA LIGI YA MKOA DAR ES SALAAM

    Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
    CHAMA cha Soka Dar es Salaam (DRFA), kimetangaza timu 18 zilizofanikiwa kutingia katika hatua ya 18 bora (raundi ya pili) ya michuano ya Ligi ya Mkoa wake.
    Timu hizo ni kutoka katika kundi (A) ambazo ni Red Coast, Yanga U20, Changanyikeni na Ukonga UTD, kundi (B) Simba U20,Stakishari,Zakhem na Beira Hotspurs,kundi (C) FFU,Sifa UTD,Pan Africa na Sinza Stars,huku  kundi (D) likitoa timu za Shababi,New Kunduchi,Ugimbi na Azania Ngano.
    Timu mbili zilizopata nafasi ya kuongezwa kwenye hatua hiyo ya pili,ni Sifa Politan FC pamoja na Tuamoyo FC,zinazokamilisha idadi ya timu 18.

    Makatibu wakuu wa timu zote 18,wanatakiwa kufika katika ofisi za DRFA zilizopo kwenye jengo la Machinga Complex Ilala (Ghorofa ya 3),siku ya jumatano 04/02/2015,saa 8 mchana,kukutana na kamati ya mshindano kwaajili ya kupata utaratibu.
    Baada ya kikao hicho DRFA itapanga makundi na kutoa ratiba ya kuanza kwa patashika hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA B ZATINGA 18 BORA LIGI YA MKOA DAR ES SALAAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top