Said Bahanuzi alimbabua shuti Ivo jana |
KIPA wa Simba SC, Ivo Mapunda sasa jicho lake halioni kabisa kwa sasa baada ya jana kupigwa na shuti la la mshambuliaji wa Yanga SC, Said Bahanuzi, Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Bahanuzi alikuwa akiichezea Polisi Moro alipotolewa na Yanga SC kwa mkopo wa kumalizia msimu na jana alikutana na mpira uliopanguliwa na Ivo Mapunda baada ya kona na kuurudisha kwa shuti kali lililombabua jichoni kipa huyo.
Ivo hakuweza kuendelea na mchezo baada ya tukio hilo dakika ya 58 na kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo alikimbizwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.
Taarifa kutoka hospitali ya Morogoro zinasema Ivo alitoka hapo jana akiwa haoni kabisa baada ya matibabu.
Baada ya matibabu ya jana, Ivo anatarajiwa kuongozana na Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe leo katika hospitali hiyo tena kwa ajili ya uchunguzi ili kujua atahitaji muda gani kabla ya kuanza tena kazi.
Ivo Mapunda baada ya kutibiwa hospitali jana mjini Morogoro |
Baada ya kuumia, Simba SC ikiwa inaongoza bao 1-0, nafasi ya Ivo ilichukuliwa na kipa chipukizi, Peter Manyika ambaye alimalizia sehemu iliyobaki ya mchezo na timu ikashinda 2-0.
Mabao ya Simba SC jana yalifungwa na Ibrahim Ajibu kipindi cha kwanza na Elias Maguri kipindi cha pili.
0 comments:
Post a Comment