MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ujerumani, Andre Schurrle ameondoka Chelsea na kujiunga na klabu ya Wolfsburg kwao kwa dau la Pauni Milioni 24.
Mjerumani huyo amesaini Mkataba wa miaka minne na inaaminika atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 85,000 kwa wiki. Nyota huyo anaondoka Chelsea baada ya kusajiliwa kwa Juan Cuadrado kutoka Fiorentina kwa dau la Pauni Milioni 27.
Kulikuwa kuna wasiwasi uhamisho wa Schurrle usingeweza kuwahi pazia la usajili la Ujerumani ambalo linafungwa saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment