// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RUVU SHOOTING YAENDELEA KUNG'ARA MLANDIZI, YAICHAPA 2-1 STAND UTD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RUVU SHOOTING YAENDELEA KUNG'ARA MLANDIZI, YAICHAPA 2-1 STAND UTD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 01, 2015

    RUVU SHOOTING YAENDELEA KUNG'ARA MLANDIZI, YAICHAPA 2-1 STAND UTD

    RUVU Shooting (pichani) imeendelea kutumia vizuri Uwanja wa nyumbani, baada ya kuifunga Stand United mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
    Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Ruvu walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Juma Nade dakika ya tano, kabla ya Hamisi Thabit kuisawazishia Stand dakika ya 53.
    Yahya Tumbo ndiye aliyeihakikishia pointi tatu za nyumbani Ruvu hivi leo, baada ya kufunga bao la pili na la ushindi dakika ya 89.
    Mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Yanga SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAENDELEA KUNG'ARA MLANDIZI, YAICHAPA 2-1 STAND UTD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top