TIMU ya Manchester United imeifunga Sunderland mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Old Trafford.
Ikiongozwa na washambuliaji Wayne Rooney na Radamel Falcao, timu hiyo ya Louis van Gaal ilicheza vizuri na kupata ushindi huo kwa mabao ya kipindi cha pili..
Refa Roger East alikuwa kituko pale alipomuonyesha kadi nyekundu Wes Brown badala ya John O'Shea aliyemuangusha kwenye eneo la hatari Radamel Falcao na kusababisha penalti.
Nahodha wa England, Rooney akaenda kuifungia bao la kwanza kwa penalty United dakika ya 66, kabla ya kufunga la pili kwa kichwa dakika ya 84 na sasa United inafikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 27.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Valencia, Smalling, Evans, Rojo, Blind; Herrera, Young, Di Maria/Januzaj, Rooney/Mata na Falcao/Fellaini.
Sunderland: Pantilimon; Reveillere, van Aanholt, Brown, O’Shea, Cattermole, Larsson, Gomez, Johnson/Fletcher, Wickham/Fletcher na Defoe/Fletcher.
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2973519/Manchester-United-2-0-Sunderland-Wayne-Rooney-answers-calls-reliable-striker.html#ixzz3T3rsBx12
0 comments:
Post a Comment