TIMU ya Atletico Madrid imeitandika mabao 4-0 Real Madrid katika mchezo wa La Liga jioni ya leo.
Mwanasoka Bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alicheza kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza adhabu yake, lakii alitoka uwanjani anazomewa na mashabiki wa wenyeji baada ya kipigo.
Kiungo wa zamani wa Chelsea, Tiago alifunga bao la kwanza dakika ya 14, Saul Niguez akafunga la pili dakika ya 18, kabla ya Antoine Griezmann kufunga la tatu dakika ya 67 na Mario Mandzukic kufunga la nne dakika ya 89 kwa pasi ya Fernando Torres.
Kikosi cha Atletico Madrid kilikuwa; Moya, Juanfran, Miranda, Godin, Siqueira, Tiago, Koke/Saul dk10/Garcia dk71, Gabi, Turan, Griezmann/Torres dk77 na Mandzukic.
Real Madrid; Casillas, Coentrao, Nacho, Varane, Carvajal, Khedira/Jese dk46, Kroos, Isco/Illaramendi dk68, Bale, Ronaldo na Benzema/Hernandez dk73.
Cristiano Ronaldo akiwa mnyonge baada ya Real Madrid baada ya Real kufungwa bao la pili katika kipigo cha 4-0 leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2943910/Atletico-Madrid-4-0-Real-Madrid-Cristiano-Ronaldo-s-game-ends-defeat.html#ixzz3R5BlwoNh
0 comments:
Post a Comment