// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PUMBA ZAANZA KUCHUJWA AFRIKA, AZAM KATIKA MECHI YA KISASI NA MERREIKH - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PUMBA ZAANZA KUCHUJWA AFRIKA, AZAM KATIKA MECHI YA KISASI NA MERREIKH - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, February 14, 2015

    PUMBA ZAANZA KUCHUJWA AFRIKA, AZAM KATIKA MECHI YA KISASI NA MERREIKH

    Na Mwandishi Wetu, CAIRO
    MSIMU mpya wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaanza wikiendi hii, timu 50 zikiingia uwanjani katika hatua ya mchujo kuwania kusonga mbele.
    Michuano hiyo inaanza mara tu baada ya kumalizka kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea, ambako Ivory Coast waliibuka mabingwa kwa kuwafunga Ghana kwa penalti 9-8 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 wiki iliyopita.
    Jumla ya klabu 57 wapo kwenye mbio za kurithi taji la ES Setif ya Algeria, lakini timu nyingine sita; Coton Sport ya Cameroon, AC Leopards ya Kongo), Al Ahly ya Misri, TP Mazembe ya DRC na CS Sfaxien na Esperance zaTunisia hazijapngwa katika hatua ya mchujo.
    Azam FC wataanza na El Merreikh ya Sudan kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam

    Timu zitakazofuzu kati ya  50 zinazoumana wikiendi hii, ndio zitakwenda kuungana na vigogo wa Afrika kuanzia hatua ya 32 Bora.
    Miongoni mwa mechi kali za Ligi ya Mabingwa ni kati ya Sewe Sport ya Ivory Coast dhidi ya AS Kaloum ya Guinea, Ahly Tripoli ya Libya dhidi ya Smouha ya Misri, Recreativo do Libolo ya Angola na Sanga Balende ya DRC, Stade Malien ya Mali dhidi ya Moghreb Tetouan ya Morocco na Azam FC ya Tanzania dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
    Azam FC ilifungwa kwa penalti 4-3 na Merreikh katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Agosti 20, mwaka jana mjini Kigali, Rwanda  baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
    na kesho timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake itakuwa inajaribu kulipa kisasi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 
    Mabingwa awa zamani wa taji hilo, Raja Athletic ya Morocco (washindi wa 1989, 1997, 1999) na Enyimba ya Nigeria (2003, 2004) pia wamo kwenye hatua ya mchujo.
    Baada ya mechi za kwanza leo mechi za marudiano zitachezwa wiki ijayo.

    RATIBA MACHUJO LIGI YA MABINGWA AFRIKA…
    Jana, Februari 13, 2015
    Al-Ahly Tripoli (Libya) Vs Smouha (Misri)
    Raja Casablanca (Morocco) Vs Diables Noirs (Kongo)
    Leo, Februari 15, 2015
    Sewe Sport (Ivory Coast) Vs AS Kaloum (Guinea)
    AS Pikine (Senegal) Vs Etoile Filante (Burkina Faso)
    Al-Hilal (Sudan) Vs KMKM (Zanzibar)
    Recreativo Libolo (Angola) Vs Sanga Balende (DRC)
    KCCA (Uganda) Vs Cosmos Bafia (Cameroon)
    Lydia Academic (Burundi) Vs Kabuscorp (Angola)
    Mouloudia El-Eulma (Algeria) Vs St George (Ethiopia)
    Gor Mahia (Kenya) Vs CNaPS Sport (Madagascar)
    Al-Malakia (Sudan Kusini) Vs Kano Pillars (Nigeria)
    Real Banjul (Gambia) Vs Barrack Young Controllers (Liberia)
    Kaizer Chiefs (Africa Kusini) Vs Township Rollers (Botswana)
    St Michel Utd (Shelisheli) Vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
    Mangasport (Gabon) Vs Bantu (Lesotho)
    Kesho, Februari 15, 2015
    Azam FC (Tanzania) Vs El-Merreikh (Sudan)
    Mbabane Swallows (Swaziland) Vs ZESCO Utd (Zambia)
    USM Alger (Algeria) Vs Foullah Edifice (Chad)
    Fomboni Moheil (Comoro) Vs Big Bullets (Malawi)
    Ela Nguema (Equatorial Guinea) Vs Semassi Sokode (Togo)
    Enyimba (Nigeria) Vs Buffles  (Benin)
    Liga Muçulmana (Msumbiji) Vs APR FC (Rwanda)
    CO Bamako (Mali) Vs Moghreb Tetouan (Morocco)
    Stade Malien (Mali) Vs AS Gendarmerie Nationale (Niger)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PUMBA ZAANZA KUCHUJWA AFRIKA, AZAM KATIKA MECHI YA KISASI NA MERREIKH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top