Na Princess Asia, MOROGORO
AZAM FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji Polisi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jioni ya leo.
Kwa matokeo hayo, Azam FC inarejea kileleni mwa Ligi Kuu baada ya kutimiza pointi 22 baada ya mechi 12, sawa na Yanga SC wanaorudi nafasi ya pili, lakini timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inapanda juu kwa wastani wa mabao.
Mabao ya Azam FC leo yamefungwa pacha kutoka nchini Ivory Coast, la kwanza Kipre Herman Tchetche dakika ya 11 na la pili Kipre Michael Balou dakika ya 68.
Mabao ya Polisi Moro, leo yamefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Edward Christopher dakika ya 29 na kiungo wa zamani wa Azam FC, Suleiman Kassim ‘Selembe’ dakika ya 81.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Simba SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Azaam Fc wametoa sare na Polisi mjini Morogoro leo |
Mabao ya Azam FC leo yamefungwa pacha kutoka nchini Ivory Coast, la kwanza Kipre Herman Tchetche dakika ya 11 na la pili Kipre Michael Balou dakika ya 68.
Mabao ya Polisi Moro, leo yamefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Edward Christopher dakika ya 29 na kiungo wa zamani wa Azam FC, Suleiman Kassim ‘Selembe’ dakika ya 81.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Simba SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
0 comments:
Post a Comment