// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PLUIJM ASEMA BDF WATAKUFA WATAKE WASITAKE TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PLUIJM ASEMA BDF WATAKUFA WATAKE WASITAKE TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 12, 2015

    PLUIJM ASEMA BDF WATAKUFA WATAKE WASITAKE TAIFA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amesema kwamba ushindi ndiyo dhamira kuu katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana mwishoni mwa wiki.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Mholanzi huyo amesema kwamba anatarajia mchezo huo utakuwa mgumu, lakini dhamira yao ni ushindi.
    “Maandalizi yetu ni mazuri, wachezaji wote wako vizuri kuelekea mchezo huo na kwa ujumla tuko tayari kama timu. Tuko tayari kupata ushindi mzuri nyumbani,”alisema.
    Kocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amesema ushindi lazima Jumamosi dhidi ya BDF

    Hata hivyo, Pluijm amesema anaamini mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa wapinzani wao ni timu nzuri pia na watapenda kupata matokeo mazuri ugenini.
    Mchezo huo utachezeshwa na refa Thierry Nkurunziza, atakayesaidiwa na Ramadhani Nijimbere namba moja, Herve Kakunze namba mbili na mezani George Gatogato, wote wa Burundi wakati Kamisaa atakuwa Joseph Nkole wa Zambia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PLUIJM ASEMA BDF WATAKUFA WATAKE WASITAKE TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top