MABONDIA Wladimir Klitschko na Bryant Jennings walikutana uso kwa uso katika jengo la Empire State jana kuelekea pambano lao litakalofanyika ukumbi wa Madison Square Garden, Aprili 25, mwaka huu.
Wawii hao walipigwa picha ghorofa ya 86 kwenye jengo hilo la kihistoria wakati wakipiga picha za promo za pambano lao litakalofanyika baadaye mwaka huu.
Klitschko, bingwa wa muda mrefu wa uzito wa juu duniani, atapigana Marekani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008, alipompiga Sultan Ibragimov katika ukumbi huo huo.
Klitschko na Jennings watapanda ulingoni Madison Square Garden Aprili 25, 2015
Wawili hao walionyesha kuheshimiana wakati wa upogaji picha za promo za pambano lao jana
0 comments:
Post a Comment