MWANASHERIA maarufu nchini Marekani, Andrea J. Cabral aliwahi kusema; “A person's First Obligation Should Be To Help The Member Of His Own Family Before He Can Begin Thinking Of Talking About Helping Others. Remember, charity begins at home,”.
Alikuwa anamaanisha kwamba, jukumu la kwanza la mtu ni kusaidia kwanza ndugu zake, watu wake, jamaa zake, kabla hajaanza kufikiria kuwasaidia wengine na akakumbushia; “hisani huanzia nyumbani,”.
Muda umepita tangu nimesoma maneno hayo ya Jaji Andrea Cabral, lakini nilijikuta nayakumbuka wiki iliyopita pamoja na maneno mengine yenye kushabihiana na hayo yaliyowahi kusemwa na watu mbalimbali.
Kilichonirudisha nyuma kukumbuka maneno ya Jaji Cabaral na mengine ya aina hiyo ni kufuatia, Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Yussuf Manji kuchangia dola za Kimarekani 500,000, kiasi cha Sh. Milioni 900 Umoja wa Afrika (AU).
Wiki mbili zilizopita, Manji alikuwa sehemu ya msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete uliokwenda Addis Ababa, Ethiopia kwenye Mkutano wa AU.
Na akiwa huko, milionea huyo mwenye asili ya Kiasia, ambaye bila ya yeye kwa sasa ‘Yanga haipumui‘ alitoa msaada huo wenye thamani ya Sh. Milioni 900 za Tanzania kusaidia vita dhidi ya maradhi ya Ebola.
Pamoja na hayo, Manji aliwasilisha pendekezo mbele ya Marais AU kuanzisha mashindano maalum ya kupambana na ugonjwa wa Ebola.
Pendekezo hilo la Manji alilitoa Alhamisi ya Januari 29 mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kulikofanyika mkutano huo.
Katibu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tibohora ambaye naye aliongozana na Manji alisema katika kikao hicho cha 24 cha AU Manji aliwasilisha pendekezo hilo akitaka nchi 54 za Afrika kushiriki katika mashindano hayo mafupi kusaka fedha za kupambana na ugonjwa huo hatari unaiosumbua Afrika Magharibi kwa kuchukua washindi wawili wa juu katika kila ligi.
Tibohora alisema katika pendekezo hilo la Manji ambalo nchi zote zililiafiki Manji ametaka mashindano hayo kuchezwa kwa kanda na kwa mfumo wa nyumbani na ugenini huku kila klabu ikitakiwa kuchangia kiasi cha dola 100, 000 kama ada ya ushiriki.
Alisema lengo la Manji ni kutaka kuona soka inachangia katika mapambano ya ugonjwa huo, akiamini kiasi cha dola Milioni 10.8 kitapatikana.
"Kwa kuwa mechi hizo zitakuwa zikiendeshwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini, Manji ameomba klabu itakayocheza nyumbani itoe nusu ya mapato ya mechi husika iende katika mapambano hayo, hapo pia klabu zitanufaika na nusu ya mapato hayo. Lakini pia, ushindani huo utazinufaisha baadhi ya nchi,”alisema Dk Tiboroha.
Wazo la Manji ni zuri na bila shaka limepokewa vizuri mno na watu mbalimbali wa Afrika, wakiwemo Marais wa Bara hili waliokutana Addis mwishoni mwa Januari.
Na zaidi, msaada wake ni mkubwa ambao anautoa katika wakati mwafaka, Ebola umekuwa ugonjwa tishio Magharibi mwa bara letu.
Ni miezi miwili iliyopita tu wakati Morocco walipojivua uenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa kuhofia misafara ya timu na mashabiki kutoka Magharibi mwa Afrika, wangeingiza maradhi ya Ebola nchini mwao.
Bahati nzuri, Equatorial Guinea ikaomba kuipokea Morocco uenyeji na hatimaye leo Fainali inachezwa, apatikane bingwa mpya wa AFCON mongoni mwa Ivory Coast na Ghana.
Kwa kuwa Manji alijitambulisha anatoka klabu ya Yanga SC ya Tanzania wakati anatoa dola hizo 500, 000 naamini hata Marais wa Afrika waliokuwepo mkutanoni wangependa kujua zaidi kuhusu klabu hiyo.
Nadhani watakwenda kupekua pekua kwenye mitandao kutafuta taarifa za klabu hiyo ilivyo sasa, chini ya Mwenyekiti aliyechangia dola 500,000 Mkutano wa AU.
Watakuta taarifa gani unadhani zaidi ya hizi ambazo sote tunajua, Yanga haina hata Uwanja wake wa mazoezi. Jengo lake halifai watu kuishi ndiyo maana wachezaji wanapelekwa kwenye hoteli nyingine kuweka kambi.
Kweli, Manji amefanya jambo zuri sana kusaidia fedha zote hizo AU, lakini tu wakati anafanya hilo kubwa, huku nyuma Yanga anayaiongoza haina Uwanja wa mazoezi tu.
Hisani ya aina hii unaweza kuiitaje? Ufahari au? Ndiyo maana nimekumbuka maneno ya Jaji Andrea Cabral.

0 comments:
Post a Comment