// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGASSA ATOA ‘BUTI’ MAALUM KWA AJILI YA BDF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGASSA ATOA ‘BUTI’ MAALUM KWA AJILI YA BDF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Friday, February 13, 2015

        NGASSA ATOA ‘BUTI’ MAALUM KWA AJILI YA BDF

        Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
        MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga SC, Mrisho Ngassa amefanya maandalizi ya kivyake kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya BDF ya Botswana kwa kuagiza kiatu maalum atakachokitumia katika mechi hiyo.
        Kiatu hicho maalum cha Ngassa kilichotengenezwa na Kampuni ya Nike ambayo pia ndiyo wadhamini wakuu wa mshambuliaji wa Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo kimeshatua kikitokea nchini Uingereza.
        Ngassa ameiambia BIN ZUBEIRY kuwa amelazimika kutumia kiasi cha shilingi 300,000 kuagiza kiatu hicho ambacho ubavuni kimeandikwa jina lake na namba 17 anayotumia katika timu hiyo.
        Mrisho Ngassa, ndilo jina la kiatu maalum alichotoa mshambulaiji huyo wa Yanga SC kwa ajili ya mchezo wa kesho 


        Mrisho Ngassa kushoto amejiandaa kikamilifu kwa ajili ya BDF kesho

        "Niliwaza nifanye nini katika mchezo huu, nikapanga kwamba nataka kuisaidia Yanga katika mechi zake hususan hizi mechi za Kimataifa ambazo msimu uliopita nilikuwa mfungaji bora,"alisema Ngassa.
        "Mbali na hilo nikapata wazo la kutafuta kiatu maalum kama ambavyo wenzetu wa Ulaya wanafanya nikaona niagize kiatu Uingereza kilichoandikwa jina langu na sasa kimefika nikipata nafasi kesho watu watakiona."
        Wakati huo huo; Uongozi wa Yanga umetoa taarifa rasmi kwamba mchezo wao wa kesho dhidi ya BDF ya Botswana hautaonyeshwa na kituo chochote cha televisheni hapa nchini.
        Hilo limetangazwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ndani ya Yanga Jerry Muro ambaye ameiambia BIN ZUBEIRY kuwa hakuna kituo chochote ndani na nje ya nchi kitakachoweza kurusha mchezo huo.
        Muro amewataka mashabiki wote wa Yanga kuachana na kusubiri mchezo huo katika luninga kwa kuwa hautaonyeshwa moja kwa moja na kituo chochote badala yake watafute tiketi mapema ili watinge Uwanja wa Taifa.
        "Hatujakubaliana lolote na kituo chochote kuweza kuonyesha mchezo wetu tunaomba tuwaambie mashabiki wote wa soka waje moja kwa moja uwanjani wadikae vibandani wala majumbani kusubiri mchezo huu katika televisheni,"amesema Muro.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: NGASSA ATOA ‘BUTI’ MAALUM KWA AJILI YA BDF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry