Na Juma Mohammed, MTWARA
TIMU pekee inayowakilisha mikoa ya kusini, Ndanda FC imemaliza raundi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara huku ikishindwa kufikia malengo iliyopanga
Akizungumzia mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo Afisa habari wa ndanda Idrisa Bandali amesema walipanga kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa nafasi tatu za juu lakini malengo hayo yamefeli huku wakiambulia nafasi ya tatu mkiani
”Tumeshindwa kufikia malengo lakini kila mtu ameona tunavyocheza tunabadilika kila mchezo ligi ya mwaka huu ni ngumu sana ila bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwani hata bingwa bado hajajulikana “ alisema Bandali.
Timu hiyo ambayo ilianza kwa mbwembwe baada ya kuanza ligi kwa kuwatandika goli nne Stand united wakiwa ugenini lakin baadae ilipoteza mvuto kwa mashabiki wake baada ya kushindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kujikuta ikiambulia pointi nne tu katika mechi nne za nyumbani
Timu hiyo kwa sasa ipo nyumbani mtwara ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa nangwanda sijaona mjini hapa tayari kujiandaa na raundi ya pili ambapo itafungua na Stand United katika mchezo utakaocheza hapahap Mtwara.

Kikosi cha Ndanda kimemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kikiwa mkiani |
Timu hiyo ambayo ilianza kwa mbwembwe baada ya kuanza ligi kwa kuwatandika goli nne Stand united wakiwa ugenini lakin baadae ilipoteza mvuto kwa mashabiki wake baada ya kushindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kujikuta ikiambulia pointi nne tu katika mechi nne za nyumbani
Timu hiyo kwa sasa ipo nyumbani mtwara ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa nangwanda sijaona mjini hapa tayari kujiandaa na raundi ya pili ambapo itafungua na Stand United katika mchezo utakaocheza hapahap Mtwara.
0 comments:
Post a Comment