Na Prince Akbar, MBEYA
WINGA wa Yanga SC, Simon Msuva jana amefunga bao lake 24 tangu amejiunga na klabu hiyo mwaka 2012 akitokea Moro United.
Simon alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 jana wa Yanga SC dhidi ya wenyeji Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Na kwa ushindi huo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC inapanda kileleni kwa kutimiza pointi 28 baada ya kucheza mechi 14, hivyo kuwazidi kwa pointi mbili mabingwa watetezi, Azam FC.
Mabao yote ya Msuva jana yalitokana na kona maridadi za kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho ambaye pia alisababisha na bao la tatu. Coutinho alipiga shuti ambalo lilimbabatiza beki wa Prisons, Lugano Mwangama na kutinga nyavuni.
Tangu amejiunga na Yanga SC, akisajiliwa kama mchezaji wa timu ya vijana kutoka Moro United, Msuva amekwishaichezea timu hiyo mechi
86.
Mabao ya Msuva jana, yalifuta ukame wa mabao wa kinda huyo uliodumu tangu Januari- kwani kwa kipindi chote hicho imeshuhudiwa akikosa mabao ya wazi.

![]() |
Simon Msuva akishangilia baada ya kufunga bao lake la 24 jana tangu ajiunge na Yanga SC mwaka 2012 |
![]() |
Andrey Coutinho ndiye alikuwa mpishi wa mabao yote ya Yanga SC jana |
![]() |
Wachezaji wa Yanga SC wakiwapongeza Msuva na Coutinho jana Sokoine |
Mabao yote ya Msuva jana yalitokana na kona maridadi za kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho ambaye pia alisababisha na bao la tatu. Coutinho alipiga shuti ambalo lilimbabatiza beki wa Prisons, Lugano Mwangama na kutinga nyavuni.
Tangu amejiunga na Yanga SC, akisajiliwa kama mchezaji wa timu ya vijana kutoka Moro United, Msuva amekwishaichezea timu hiyo mechi
86.
Mabao ya Msuva jana, yalifuta ukame wa mabao wa kinda huyo uliodumu tangu Januari- kwani kwa kipindi chote hicho imeshuhudiwa akikosa mabao ya wazi.
0 comments:
Post a Comment