// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MRISHO NGASSA AWAINUA TENA YANGA, APIGA ZOTE MBILI MTIBWA IKIFA 2-0 TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MRISHO NGASSA AWAINUA TENA YANGA, APIGA ZOTE MBILI MTIBWA IKIFA 2-0 TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 08, 2015

    MRISHO NGASSA AWAINUA TENA YANGA, APIGA ZOTE MBILI MTIBWA IKIFA 2-0 TAIFA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Shukrani kwake, mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa aliyetokea benchi na kufunga mabao yote kipindi cha pili na sasa Yanga SC inafikisha pointi 25 baada ya mechi 13, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam wenye pointi 22 za mechi 12.
    Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Israel Nkogo wa Dar es Salaam, aliyesaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya na Josephat Bulali wa Tanga, dakika 45 za kwanza zilimalizika kukiwa hakuna mabao.
    Mrisho Ngassa kushoto akishangilia Simon Msuva baada ya kufunga leo

    Washambuliaji wa Yanga SC, Amisi Tambwe, Kpah Sherman, Andrey Coutinho na Simon Msuva wote kila mmoja alikosa bao la wazi kipindi hicho.
    Yanga SC ilipata pigo dakika ya 39 baada ya beki wake kushoto, Edward Charles kuumia na kutoka nje, nafasi yake ikichukuliwa na Juma Abdul.
    Kipindi cha pili, mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kumtoa Mliberia Sherman na kumuingiza Ngassa yaliizindua Yanga SC na kupata mabao mawili ndani ya dakika saba.
    Mshambuliaji wa Yanga SC, Amisi Tambwe akimruka kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed aliyedaka mpira chini. Kushoto ni beki Salim Mbonde
    Kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi akimdhibiti beki wa Yanga SC, Mbuyu Twite
    Winga wa Yanga SC, SImon Msuva akimtoka kiungo wa Mtibwa, Ibrahim Rajab Jeba

    Kabla ya Ngassa kufunga, aliwakosakosa Mtibwa Sugar katika mpira wa kwanza tu kugusa baada ya kuingia dakika ya 53, akipiga vizuri mpira wa juu uliotoka nje sentimita chache. 
    Dakika ya 55 Ngassa akafunga bao la kwanza akimalizia krosi ya Simon Msuva na dakika ya 62 akafunga la pili akiwatoka mabeki wa Mtibwa na kumlamba chenga kipa Said Mohammed kabla ya kuutumbukiza mpira nyavuni.
    Tangu hapo, Ngassa akachangamka zaidi uwanjani na kuwa mwiba kwa mabeki wa Mtibwa Sugar.
    Kikosi Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Edward Charles/Juma Abdul dk39, Rajab Zahir, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Kpah Sherman/Mrisho Ngassa dk53 na Andrey Coutinho/Hussein Javu dk83.
    Mtibwa Sugar; Said Mohammed, Andrew Vincent, David Luhende, Ally Lundenga, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Ally Sharrif/Ramadhani Kichuya dk62, Henry Joseph, Ame Ally, Ibrahim Rajab Jeba/Mohammed Ibrahim dk27 na Jamal Mnyate/Vincent Barnabas dk60.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MRISHO NGASSA AWAINUA TENA YANGA, APIGA ZOTE MBILI MTIBWA IKIFA 2-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top