KOCHA Jose Mourinho amesema kwamba mchezaji wake, Eden Hazard ameomba kutengenezewa 'shin pad' (kizuia ugoko) maalum ili kuulinda mguu wake mfupi kwa sababu amekuwa akichezewa rafu sana na mabeki.
Hazard alichezewa rafu mara tisa Chelsea ikimenyana na Paris St Germain Jumanne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na bado Mbelgiji huyo ndiye mchezaji anayechezewa rafu nyingi katika Ligi Kuu ya England.
Winga huyo amechezewa rafu mara 74 katika Ligi Kuu - hiyo ikiwa ni mara 14 zaidi ya mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling - wakati akijiandaa kuingia kwenye mechi dhidi ya Burnley Uwanja wa Stamford Bridge Jumamosi.
Winga wa Chelsea, Eden Hazard alichezewa rafu tisa Jumanne katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG
Mourinho amesema: "Eden ameniomba nizungumze na baadhi ya watu marafiki zangu wanaotengeneza shin-pads za kuenea mguu mzima. Anataka kuukinga mguu wake wote. Kama farasi,".
"Kwa kawaida, unapochezewa rafu 100, wapinzani watapata kadi za njano za wastani unaoendana.
"Hivyo, kama ndiye mchezaji anayeoongoza kuchezewa rafu nyingi, lazima pia awe mchezaji anayewaponza wachezaji wengi wa timu pinzani kupata kadi za njano. Lakini si hivyo,".
Mourinho anaamini kwamba mshambuliaji huyo, ambaye amesaini Mkataba mpya wa miaka mitano unaomfanya 'akunje' mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki, amekuwa akiwindwa zaidi ndani na nje.
0 comments:
Post a Comment