Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA kipa wa Yanga SC, Juma Kaseja leo asubuhi amepandishwa Baraza la Usuluhishi katika mahakama ya Kazi, Dar es Salaam kuhusu mashataka ya kuvunja mkataba na klabu hiyo, lakini tukio la moto limeahirisha shauri hilo.
Akizungumza mara baada ya kusikilizwa kwa awali kwa shauri hilo Mwanasheria wa Yanga SC, Frank Chacha amesema shauri hilo limeahirishwa kufuatia maombi ya upande wa Kaseja ambao ofisi zao za Kampuni ya Kisheria ya Mbamba Advocate zimeungua moto.
Sehemu ya majengo ambayo ofisi za Mbamba Advocate ziliungua jengo hilo lipo pale Mnazi mmoja
Chacha amesema Kaseja ambaye alikuwepo na mwanasheria wake, Nestory Mwenda waliwasilisha maombi hayo mbele ya Mheshimiwa Fimbo kuwa nyaraka zao mbalimbali za shauri hilo kuungua na moto katika ofisi zao zilizoungua na moto hivi karibuni katika jengo la Consolidated Investments lililopo mtaa wa Libya Mnazi mmoja.
"Tumelazimika kuwakubalia maombi yao hayo kwa kuwa hata sisi tunafahamu kwamba wenzetu wamekumbana na hilo tatizo sasa tnasububiri wajikamilishe ili turudi tena katika tarehe ambayo kesi imepangwa kuendelea,"alisema Chacha.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea Machi 10 ambapo kila upande umekubaliana kuwa utakuwa tayari kuendelea kwa shauri hilo.
Yanga imemfikisha Kaseja katika kesi hiyo kwa madai kwamba kipa huyo mkongwe alivunja mkataba wake kwa kitendo cha kugoma kendelea kukipiga na klabu hiyo ambapo katika madai hayo klabu hiyo imemtaka Kaseja kulipa fidia ya shilingi 340 milioni.

Aliyekuwa kipa wa Yanga Juma Kaseja (kulia)akijadiliana jambo na wakili wake Nestory Mwenda kutoka Kampuni ya Mbamba Advocate,katika Baraza la Usuluhishi katika Mahakama ya Kazi jijini Dar es Salaam
Sehemu ya majengo ambayo ofisi za Mbamba Advocate ziliungua jengo hilo lipo pale Mnazi mmoja
Chacha amesema Kaseja ambaye alikuwepo na mwanasheria wake, Nestory Mwenda waliwasilisha maombi hayo mbele ya Mheshimiwa Fimbo kuwa nyaraka zao mbalimbali za shauri hilo kuungua na moto katika ofisi zao zilizoungua na moto hivi karibuni katika jengo la Consolidated Investments lililopo mtaa wa Libya Mnazi mmoja.
"Tumelazimika kuwakubalia maombi yao hayo kwa kuwa hata sisi tunafahamu kwamba wenzetu wamekumbana na hilo tatizo sasa tnasububiri wajikamilishe ili turudi tena katika tarehe ambayo kesi imepangwa kuendelea,"alisema Chacha.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea Machi 10 ambapo kila upande umekubaliana kuwa utakuwa tayari kuendelea kwa shauri hilo.
Yanga imemfikisha Kaseja katika kesi hiyo kwa madai kwamba kipa huyo mkongwe alivunja mkataba wake kwa kitendo cha kugoma kendelea kukipiga na klabu hiyo ambapo katika madai hayo klabu hiyo imemtaka Kaseja kulipa fidia ya shilingi 340 milioni.
0 comments:
Post a Comment