MANCHESTER United imeponea chupuchupu kulala mbele ya West Ham United baada ya kuata sare ya 1-1 ugenini usiku huu.
Cheikhou Kouyate aliifungia West Ham bao la kuongoza dakika ya 49 na United wakahaha tangu hapo kusaka bao la kusawazisha hadi kuelekea kupoteza mchezo.
Hata hivyo, kiungo Daley Blind akawanusuru Mashetani Wekundu kulala baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 90.
Man United ilipata pigo baada ya beki wake Luke Shaw kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekndu. Pamoja na matokeo hayo, Man United wanabaki nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, wakati West Ham wanabaki nafasi ya nane.
Daley Blind (kushoto) akishangilia baada ya kuisawazishia Manchester United leo
Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2944770/West-Ham-1-1-Manchester-United-Daley-Blind-s-injury-time-strike-cancels-Cheikhou-Kouyate-opener-rescue-visitors-point.html#ixzz3RBHOXpc1
0 comments:
Post a Comment