KUNA wakati fulani sura ya onyesho ilibadilika kidogo na pengine kama mtu ndo angekuwa anaingia ukumbini muda huo basi angedhani yupo harusini.
Naam, Luizer Mbutu na mumewe Fariala Mbutu walichukua muda mrefu jukwaani wakipozi kwa picha na kupokea zawadi mbali mbali huku baadhi ya nasaha zikielekezwa juu ya ndoa yao.
Hilo ni onyesho la miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta lililofanyika ndani ya ukumbi wa Mango Garden juzi Jumamosi.
Lilikuwa ni onyesho lililovuta hisia za watu wengi, kwa hikika lengo la tukio lilikuwa zuri sana na ni kitu kinachostahili pongezi.
Kukaa kwenye bendi moja kwa miaka 16 si mchezo, Luizer na wamiliki wa Twanga Pepeta wameonyesha ni namna gani wameweza kuvumiliana na kuvuka milima na mabonde pamoja katika kusukuma mbele gurudumu la bendi hiyo. Hakuna ubishi kuwa Luizer ni nembo ya Twanga Pepeta.
Maandalizi onyesho yalikuwa mazuri kuanzia matangazo hadi kuboresha mandhari ya ukumbi wa Mango Garden, madhurio ya mashabiki yalikuwa ni makubwa sana na inatia moyo kuwa kumbe muziki wa dansi bado unapendwa.
Nivutiwa sana na namba Luizer alivyoanza ratiba yake ya burudani – wimbo “Mama Kioo cha Familia” na “Kuolewa” ilikuwa ni kitu kitamu sana.
Lakini pamoja na mazuri yote ya onyesho hilo, yako mapungufu kadhaa kwenye kwenye tamasha hilo ambayo hayawezi kuachwa yapite hivi hivi.
Lile lilikuwa ni onyesho la burudani, watu wamelipa ili kwenda kupata burudani, matukio yoyote yasiyo ya kibrudani yalipaswa kufupishwa sana. Kutumika takriban saa nzima mfululizo kwa mambo ambayo si ya kiburudani ilikuwa ni kosa la kiufundi.
Vyombo vilivyotumika vinakidhi maonyesho ya kawaida ya kila Jumamosi lakini kwa tamasha kama lile. Hakika ‘sound’ haikuwa nzuri na haikidhi viwango vya maonyesho kama yale.
Wasindikizaji kibao hawakuonekana, hili nalo ni tatizo. Katika matangazo ya onyesho hilo tulitajiwa uwepo wa Khadija Kopa, Mwasiti, Recho na Linah ambo wote hawakuwepo, hii ni aina fulani ya ubabaishaji. Hao wote ni wasanii wenye majina makubwa na inawezekana kabisa wapo mashabiki waliowafuata wasanii hao na hivyo kitendo cha kutokuwepo kwao bila maelezo yoyote, inakuwa ni dosari nyingine katika onyesho hilo.
Mpangilio wa matukio jukwaani ulikuwa una mushkel. Kuna vitu vilikuwa vinafanyika jukwaani kama vile hakukuwa na muongozo maalum, kuna wakati hata MC wa onyesho hilo Sakina Lioka alionekana kuyumba au kuyumbishwa.
Nilitegemea zaidi kumuona Luizer akiwa mburudishaji kuliko kuwa muongeaji au muongozaji wa shughuli, pengine ingependeza shukran za Luizer zingeandikwa kama risala fupi na akapewa mtu mwingine aisome kwa niaba yake hata kabla ya mwimbaji huyo kuonekana jukwaani.
Hata zawadi zake alizopewa na watu mbali mbali zingeweza kuwekwa kwenye eneo kwenye eneo maalumu na kisha zitangazwa kwa kifupi jukwaani pale hata kwa kumtumia MC badala ya kupandisha kila mmoja mwenye zawadi – yalikuwa ni matumizi mabaya ya muda.
Mume wa Luizer (Fariala Mbutu) ni mwanamuziki, nadhani ingefurahisha zaidi kama angepanda jukwaani na kushika gitaa wakati mkewe anaimba kuliko kwenda kuungana na Luizer katika ratiba ya kupokea zawadi.

0 comments:
Post a Comment