TIMU ya Bercelona, imeichapa mabao 5-2 Athletic Bilbao katika mchezo wa La Liga usiku huu na kupunguza pengo la pointi wanazozidiwa na vinara, Real Madrid hadi kubaki moja.
Lionel Messi alifunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu dakika ya 15 kabla ya Luis Suarez kufunga la pili dakika ya 26, De Marcos akajifunga kuipatia Barca bao la tatu dakika ya 62, Neymar akafunga la nne dakika ya 64 na Pedro la tano dakika ya 86.
Mabao ya Athletic Bilbao yalifungwa na Mikel Rico dakika ya 59 na Aduriz dakika ya 66, wakati timu hiyo ilipata pigo dakika ya 75, baada ya mchezaji wake, Etxeita kutolewa kwa kadi nyekundu 75.
Kikosi cha Athletic Bilbao kilikuwa: Iraizoz, De Marcos, Etxeita, Laporte, Balenziaga/Aurtenetxe dk52, San Jose, Mikel Rico, Susaeta/Benat dk69, Lopez, Muniain/Gurpegui dk78 na Aduriz.
Barcelona: Bravo, Alves/Adriano dk69, Mathieu, Pique, Alba, Xavi/Rafinha dk74, Busquets, Rakitic, Messi, Suarez/Pedro dk80 na Neymar.
Xavi (kulia) akishangilia na Messi (katikati) na Suarez kushoto baada ya ushindi wao
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2945080/Athletic-Bilbao-2-5-Barcelona-Lionel-Messi-Neymar-Luis-Suarez-target-Luis-Enrique-s-men-close-gap-Real-Madrid-La-Liga-one-point.html#ixzz3RCNwMBL1
0 comments:
Post a Comment