// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MASHUJAA WAJA NA BONANZA LA KILA JUMAPILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MASHUJAA WAJA NA BONANZA LA KILA JUMAPILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, February 17, 2015

    MASHUJAA WAJA NA BONANZA LA KILA JUMAPILI

    Na Asha Said, DAR ES SALAAM
    BENDI Bora ya muziki wa dansi Tanzania mwaka 2013/14, Mashujaa Music Band 'Wanakibega'  kila Jumapili watakuwa wanafanya bonanza maalum, katika ukumbi wa Mashujaa Lounge (zamani Business Park), uliopo Victoria Dar es Salaam.
    Mkurugenzi wa mawasiliano wa bendi hiyo Maxmilian Luhanga, alisema kuwa bendi hiyo, itakuwa na onesho hilo maalum la bonanza a, ambalo kutakuwa na michezo kwa watoto.
    Kiongozi wa Mashujaa Band, Chaz Baba kushoto

    Alisema kuanzia saa 8, mchana wazazi wanaoweza kuleta watoto wao ambao wataingia bure kucheza michezo ya watoto ambayo itakuwa kwenye ukumbi huo, ambao sasa upo chini yao.
    Luhanga alisema wameingia mkataba na sasa ukumbi huo upo chini yao, ambao watakuwa wakifanya onesho maonesho mawili kwa wiki moja katika ukumbi huo.
    Alisema Ijumaa kutakuwa na onesho lao la kawaida ambalo litafanyika kwenye ukumbi huo wakati Jumapili kutakuwa na bonanza.
    "Tumeuchukua ukumbi huo ambao sasa utaitwa Mashuja Lounge, na kutauzindua Februali 27, mwaka huu"alisema Luhanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHUJAA WAJA NA BONANZA LA KILA JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top