Shabiki wa klabu ya Fayernoord akivuja damu baada ya kupigwa na Polisi mjini Rome Italia kufuatia kufanya vurugu kuelekea mchezo wao na wenyeji Rome. Mashabiki 6,000 wa Feyenoord walisafiri hadi mji Mkuu wa Italia kutazama timu yao ikimenyana na Roma na 33 kati yao walikamatwa na katika vurugu za Jumatano, lakini 10 waliachiwa mara moja.
Mashabiki wanane wa Feyenoord walipigwa fani ya Eurio Pauni 33,000 na kufungiwa kuingia kwenye viwanja vya mechi. Mapambano zaidi yaliendelea baina ya Polisi na mashabiki hao wakati wa mechi Alhamisi na askari 17 walijeruhiwa pia, timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Olympico, mabao ya Gervinho naColin Kazim-Richards .
0 comments:
Post a Comment