MANCHESTER United imetoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 3-1 hivyo kutinga Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Preston Noth End usiku huu na sasa watakutana na mabingwa watetezi, Arsenal.
Scott Laird alitangulia kuwafungia wenyeji, Preston dakika ya 47 akimtungua kwa shuti la kubabatiza kipa David de Gea, kabla ya Ander Herrera kuisawazishia United dakika ya 65 akifumua shuti lililowapita mabeki wa Preston na kipa wao.
Marouane Fellaini akaifungia bao la pili Manchester United dakika ya 72, kabla ya Wayne Rooney kusababisha penalti dakika za lala salama na kwenda kufunga mwenyewe.
Fellaini akishangilia baada ya kuifungia Man United bao la pili
Sasa Man United itakutana na mabingwa watetezi wa Kombe la FA, Arsenal katika Robo Fainali Uwanja wa Old Trafford.
Mechi nyingine za Robo Fainali zinatarajiwa kuwa kati ya Liverpool na Blackburn, Bradford na Reading na Aston Villa dhidi ya West Brom. Mechi za Robo Fainali Kombe la FA zinatarajiwa kuchezwa Machi 7 na 8, mwaka huu.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Valencia, Smalling, Rojo, Shaw, Blind, Herrera, Fellaini, Di Maria/Rooney na Falcao/Young dk60.
Preston; Stuckmann, Humphrey, Huntington, Clarke, Wright/Wiseman dk75, Welsh, Kilkenny/Reid dk75, Gallagher, Laird, Davies/Robinson dk75 na Garner.
0 comments:
Post a Comment