KLABU ya Manchester City imemuengua katika kikosi chake cha Ligi ya Mabingwa Ulaya Stevan Jovetic ili kumuingiza Wilfried Bony.
Nyota huyo wa Montenegro, alisajiliwa kutoka Fiorentina kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 22 mwaka 2013, sasa anaweza kuwa anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo baada ya kuchaguliwa kumpisha Bony aliyesajiliwa dirisha dogo kwa Pauni Milioni 20 kutoka Swansea City.
Jovetic, ambaye amekuwa akiandamwa na majeruhi tangu atue Man City ameanza katika mechi 18 tu ndani ya miezi 19.
Stevan Jovetic ametemwa kikosi cha Ligi ya Mabingwa Manchester City
Wilfried Bony amechukua nafasi yake katika kikosi hicho
0 comments:
Post a Comment