// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MALINZI KAMISAA MECHI YA IVORY COAST NA AFRIKA KUSINI FAINALI ZA U17 AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MALINZI KAMISAA MECHI YA IVORY COAST NA AFRIKA KUSINI FAINALI ZA U17 AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 15, 2015

    MALINZI KAMISAA MECHI YA IVORY COAST NA AFRIKA KUSINI FAINALI ZA U17 AFRIKA

    FAINALI za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zinaanza leo mjini Niamey, Niger, wakati kesho Ivory Coast ikifungua dimba na Afrika Kusini, mechi ambayo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa Kamisaa.
    Mechi za ufunguzi leo ni kati ya wenyeji Niger dhidi ya Nigeria Saa 9:00 Alasiri kwa saa za huko na Saa 11:00 kwa Saa za Afrika Mashariki, wakati mchezo wa pili utakuwa kati ya Guinea na Zambia Saa 12:00 za huko na Saa 2:00 kwa saa za kwetu.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi (katikati) akiongoza kikao cha kabla ya mechi baina ya Ivory Coast na Afrika Kusini leo katika hoteli ya Gaweye mjini Niamey, Niger
    Viongozi wa Afrika Kusini katika kikao cha kabla ya mechi na jezi zao
    Viongozi wa Ivory Coast katika kikao cha kabla ya mechi leo

    Mchezo wa Ivory na Afrika Kusini, utafuatiwa na mchezo kati ya Mali na Cameroon kesho.
    Michuano hiyo ya U17 Afrika itaanza leo hadi Machi 2, mwaka huu na timu zitakazofanikiwa kutinga Nusu Fainali, moja kwa moja zitakuwa zimejikatia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia nchini Chile baadaye mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI KAMISAA MECHI YA IVORY COAST NA AFRIKA KUSINI FAINALI ZA U17 AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top