MWANAMUZIKI nguli, Lady Madonna jana alimalizia vibaya shoo yake nzuri ya kukumbukwa baada ya kuanguka kwenye ngazi jukwaani, kufuatia kusukumwa na dansa wake wakati akitumbuiza katika tuzo za Uingereza 'BRIT Awards 2015'.
Wakati akimalizia malizia kuimba wimbo Living For Love, ghafla Madonna akashindwa kuikusanya miguu yake na kuporomoka chini wakati akipishana na dansa wake katika ngazi za jukwaa la ukumbia wa London's 02 Arena.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 56 alishituka baada ya kuanguka na kuacha kuimba kwa muda, lakini akajikusanya kusanya na kuinuka kisha kuendelea na shoo yake hadi mwisho.
Mwanamuziki gwiji, Madonna akiwa ameanguka jukwaani usiku wa jana katika tuzo za Uingereza
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/tvshowbiz/article-2969176/Taylor-Swift-puts-incredibly-sexy-display-short-black-jumpsuit-fishnets-opens-BRIT-Awards-live-show.html#ixzz3SoTN2rnw
0 comments:
Post a Comment