MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wameibuka leo na kushinda mabao 4-1 dhidi ya Stoke Uwanja wa Britannia huo ukiwa ushindi wa kwanza tangu mwaka mpya.
Sergio Aguero aliwafungia wageni bao la kwanza dakika ya 33, kabla ya Peter Crouch kuisawazishia timu ya Mark Hughes dakika ya 38, hilo likiwa bao lake la sita msimu huu.
City ikapata bao la pili dakika ya 10 kipindi cha pili kupitia kwa James Milner, kabla ya Aguero kufunga la tatu kwa penalti dakika ya 55 na Samir Nasri la nne dakika ya 76.
Kiungo, Nasri akishangilia baada ya kuifungia Man City bao la nne
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2949794/Stoke-City-1-4-Manchester-City-Sergio-Aguero-double-leads-Manuel-Pellegrini-s-win-New-Year-s-Day.html#ixzz3RTj3Q8Q1
0 comments:
Post a Comment