LIVERPOOL imetinga Raundi ya Tano ya Kombe la FA baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Bolton Wanderers jana.
Eidur Gudjohsen aliifungia Bolton bao la kuongoza penalti dakika ya 59, baada ya kinda wa miaka 19, Zach Clough kuchezewa faulo na beki wa Liverpool, Martin Skrtel.
Raheem Sterling akaisawazishia Liverpool dakika ya 85, kabla ya Philippe Coutinho kufunga la ushindi dakika ya 90.
Bolton ililazimika kucheza pungufu kwa dakika 20 za mwisho baada ya mchezaji wake, Neil Danns kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na Liverpool sasa itamenyana na Crystal Palace katika Raundi ya Tano.
Kikosi cha Bolton kilikuwa; Lonergan, Dervite, Wheater, Ream, Feeney, Vela, Danns, Moxey, Clough/Trotter dk72, Gudjohnsen na Mills.
Liverpool; Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Markovic/Borini dk62, Allen, Gerrard, Moreno, Coutinho, Sterling na Lallana/Henderson dk55.
Philippe Coutinho akishangilia bao lake la dakika ya 90 katika ushindi wa Liverpool wa 2-1 dhidi ya Bolton
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2940011/Bolton-Wanderers-1-2-Liverpool-Late-goals-Raheem-Sterling-Philippe-Coutinho-cancel-Eidur-Gudjohnsen-penalty.html#ixzz3Qq39Eez8
0 comments:
Post a Comment