// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIGI YA MKOA DAR YASHIKA KASI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIGI YA MKOA DAR YASHIKA KASI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 16, 2015

    LIGI YA MKOA DAR YASHIKA KASI

    Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
    LIGI ya mkoa wa Dar es salaam inaendelea tena wiki hii kwa timu 8 kushuka katika viwanja tofauti,kupambana ili kuusaka ubingwa huo pamoja na kupata nafasi ya kuingia katika ligi daraja la pili taifa.
    Mechi za leo Februari 16,2015/Azania Ngano watakipiga dhidi ya Yanga U20 (Katika uwanja wa Karume),Stakishari watacheza na FFU (uwanja wa B.Mkapa),Changanyikeni wataumana dhidi ya Tuamoyo (uwanja wa MWL/Nyerere) na New Kunduchi wataoneshana kazi dhidi ya Sinza Stars (uwanja wa Kines).
    Pan African ilikuwa tishio mwishoni mwa miaka ya 1970 hadi 1980, kabla ya kupoteza makali yake na sasa inasota katika Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam 

    Kivumbi hicho kitaendelea tena kesho Kutwa Februari 18,2015 kwa Simba U20 kucheza na Ukonga UTD (Uwanja wa karume),Red Coast watacheza dhidi ya Shababi (MWL/Nyerere), Zakhem watacheza na Sifa UTD ( Uwanja wa Bandari) na Beirahotspurs watakipiga dhidi ya Pan African (uwanja wa Kines).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI YA MKOA DAR YASHIKA KASI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top