PAMBANO la ngumi la utajiri mkubwa duniani rasmi litakuwepo, baada ya bondia Floyd Mayweather kuposti nakala ya Mkataba aliosaini na mpinzani wake, Manny Pacquiao katika mtandao wa kijamii Ijumaa usiku.
Pambani hilo linatarajiwa kuwa thamani ya Pauni Milioni 200, linatarajiwa kufanyika Mei 2, mwaka huu nchini Marekani, nyumbani kwa Mayweather mjini Las Vegas katika ukumbi maarufu wa Grand in Las Vegas.
Wawili hao wamekuwa na uhasama wa muda mrefu, kabla ya hivi karibuni kukitana kwenye Uwanja wa mpira wa kikapu na kufanya mazungumzo, hatimaye kukubaliana na kwa mazungumzo ya pambano.
Floyd Mayweather hatimaye amethibitisha atapambana na Manny Pacquiao ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas Mei 2
Mayweather ameposti nakala ya Mkataba aliosaini kwa ajili ya pambano hilo
0 comments:
Post a Comment