// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KOPUNOVIC AWAPA NENO WACHEZAJI SIMBA SC, TENA LA HEKIMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KOPUNOVIC AWAPA NENO WACHEZAJI SIMBA SC, TENA LA HEKIMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 12, 2015

    KOPUNOVIC AWAPA NENO WACHEZAJI SIMBA SC, TENA LA HEKIMA

    Na Samira Said, MOROGORO
    KOCHA Mkuu wa Simba Mserbia, Goran Kopunovic, amewataka wachezaji wa timu hiyo kutojikuza na badala yake wanatakiwa kupambana na kujituma kwa lengo la kushinda mechi za ligi ili wapate mafanikio.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini Morogoro Kopunovic alisema juhudi na kila mchezaji kufahamu majukumu yake ndiyo silaha pekee itakayowapa mafanikio na hatimaye kutimiza ndoto.
    Alisema kuwa anawakumbusha wachezaji wake kutoidharau timu yoyote katika ligi hiyo ambayo mechi zote wanazocheza zina ushindani.
    Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic kushoto akiwa na wachezaji wake

    " Ligi ni ngumu na ina ushindani, nawaeleza mara kwa mara wajitume na wajue kwamba wao bado wako chini na hakuna anayepaswa kujiona  ni bora", alisema Kopunovic.
    Kocha huyo naye aliungana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van der Pluijm, kuuponda Uwanja wa Jamhuri kuwa hauna ubora na unasumbua wachezaji wake kucheza soka la kuburudisha.
    Kopunovic pia aliuponda uwanja wa Mkwakwani Tanga kuwa unafanya wachezaji wacheze kulingana na miundombinu ya uwanja huo na si vile walivyofundishwa.
    Simba iko mkoani Morogoro tangu jana kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Polisi Morogoro ambayo inatarajiwa kufanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani humo.
    Wenyeji Polisi Morogoro wanaofundishwa na Adolph Rishard watashuka dimbani wakiwa na pointi 18 wakati Simba wana pointi 17.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOPUNOVIC AWAPA NENO WACHEZAJI SIMBA SC, TENA LA HEKIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top