BEKI wa Liverpool na Ivory Coast, Kolo Toure ametangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya kuitumikia Tembo kwa miaka 15.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 amecheza Fainali tatu za Kombe la Dunia na saba za Kombe la Mataifa ya Afrika tangu aanze kucheza timu ya taifa mwaka 2000.
Baada ya kufungwa katika katika fainali mbili za AFCON, hatimaye Kolo alitimiza ndoto zake za kuinua ndoo ya Mataifa ya Afrika baada ya Ivory Coast kuishinda Ghana kwa matuta michuano ya mwaka 2015, wiki iliyopita nchini Equatorial Guinea.
Beki wa Ivory Coast, Kolo Toure akifurahia na Kombe la Mataifa ya Afrika wiki iliyopita baada ya kuifunga Ghana kwa penalti 9-8 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120
0 comments:
Post a Comment